Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Wanawake 35 watekwa nyara wakitoka harusini

Wanawake Nigeria Kutekwa Nigeria: Wanawake 35 watekwa nyara wakitoka harusini

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wenye silaha wamewateka nyara takriban wanawake 35 waliokuwa wakirejea makwao kutoka kwenye harusi katika Jimbo la Katsina kaskazini-magharibi mwa Nigeria. Tukio hilo linahesabiwa kuwa utekaji nyara mkubwa zaidi wa hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi yaliyoshuhudiwa nchini humo.

Msemaji wa polisi ya Nigeria, Abubakar Aliyu amesema kuwa watu wanaoshukiwa kuwa majambazi waliwavizia na kuwateka nyara takriban wanawake 35 walipokuwa wakirejea makwao kutoka kwenye harusi katika eneo la Sabuwa, usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita.

Kamishna wa Usalama wa Ndani wa Jimbo la Katsina, Nasiru Muaz amedokeza kuwa idadi ya watu waliotekwa nyara wakiandamana na bibi harusi nyumbani kwake inaweza kuwa kubwa zaidi, na kuna uwezekano kwamba watu 53 walitekwa nyara.

Ameongeza kuwa, ni hatari sana kwa msafara wa wanawake wanaombeba bibi harusi kusafiri gizani katika eneo maarufu kwa ujambazi, na kuongeza kuwa watu wenye silaha walitumia fursa hiyo na kuwateka nyara.

Polisi wa Nigeria wanaendelewa kuwatafuta wanawake waliotekwa nyara.

Vitendo vya utekaji nyara kwa ajili ya kutaka fidia ni tatizo kubwa nchini Nigeria, na magenge ya wahalifu yanafanya utekaji nyara kwenye barabara kuu, majumbani na shuleni.

Utekaji nyara ulianza kuwa tatizo kubwa nchini Nigeria mwanzoni mwa milenia ya tatu, lakini wataalamu wanahusisha ongezeko la hivi karibuni la matukio haya na mgogoro wa kiuchumi ambao unayasukuma baadhi ya makundi kwenye kufanya vitendo vya uhalifu ili kupata pesa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live