Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Wanafunzi wa kike ruhusa kuvaa hijab

Screenshot 2022 06 18 At 16.32.30 660x400.png Wanafunzi wa kike ruhusa kuvaa hijab

Sat, 18 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya juu zaidi nchini Nigeria imetoa uamuzi wa kuwaruhusu Wanafunzi wa kike wavae Hijab bila kusumbuliwa au kubaguliwa.

Serikali ya jimbo la Lagos ilikuwa imepiga marufuku matumizi ya Hijab ikidai kuwa sio sehemu ya sare za Shule zilizoidhinishwa za Wanafunzi.

Marufuku hiyo ilipingwa na wanafunzi Waislamu mwaka 2015, waliosema kuwa marufuku hiyo inakiuka haki zao za mawazo, za kidini na za elimu, mvutano wa kisheria kuhusiana na marufuku hiyo umedumu kwa muda wa miaka saba.

Uamuzi wa Mahakama hiyo ya juu zaidi nchini Nigeria hatimaye unaweza kumaliza utata huo uliowaathiri zaidi Wanafunzi katika Shule zisizo za kidini nchini Nigeria ambapo Mahakama imesema kuzuai Hijab ni kuwabagua Wanafunzi Waislamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live