Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Waandamana kuuunga mkono Palestina

Nigeria Palestina Nigeria: Waandamana kuuunga mkono Palestina

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi Waislamu wa jimbo la Bauchi nchini Nigeria kwa mara nyingine tena wameandamana na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa palestina hasa wa Ukanda wa Gaza.

Waislamu hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamesikika wakipiga nara za kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakiwa wamebeba bendera za Palestina, Waislamu hao wamemtaka Rais wa nchi hiyo Bola Ahmed Tinubu kumtimua haraka iwezekanavyo kutoka Abuja balozi wa utawala haramu wa Israel.

Kadhalika waandamanaji hao wameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua zaa haraka za kuhitimisha mauaji na jinai za Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza huko Palestina. Wananchi wa Nigeria wakiandamana kuunga mkono Palestina na kulaani jinai za Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina

Baadhi ya waandamanaji hao wamesisitiza kuwa, balozi wa Israel nchini Nigeria ni lazima afukuzwe nchini humo.

Jana Waislamu na waungaji mkono wa Palestina katika mji wa Kano, Nigeria waliandamana pia na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina hasa wa Ukanda wa Gaza.

Waislamu nchini Nigeria wamekuwa wakiandamana kila mara na kusisitiza uungaji mkono wao mkubwa kwa wananchi wa Palestina na muqawama wao dhidi ya uvamizi wa Israel na jinai zake.

Maandamano kama hayo yamekuwa yakishuhudiwa pia katika mataifa mengine ya dunia ambapo waandamanaji wanalaani jinai za Israel na himaya na uungaji mkono wa madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani kwa jinai za utawala huo ghasibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live