Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Vyama vikuu vya wafanyikazi vimeitisha mgomo wa kitaifa

Mgomo Nigeriaaa.png Nigeria: Vyama vikuu vya wafanyikazi vimeitisha mgomo wa kitaifa

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Nigeira, vyama vikubwa viwili vya wafanyikazi vimewataka wanachama wao kushiriki mgomo na kusalia nyumbani kuanzia leo Jumanne wakati huu mgomo wa kitaifa ukirejelewa.

Mgomo huu unafanyika licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama linalowazuia kufanya hivyo.

Vyama vya Nigeria Labour Congress (NLC) na Trade Union Congress (TUC) vimesema vimechukua hatua hiyo kutokana na kuendelea kupanda kwa gharama ya maisha na kuongezeka kwa bei za mafuta.

Vyama hivyo vimekuwa vikimshinikiza rais Tinubu kurejesha ruzuku kwa bidhaa za petroli, mapango wanaosema ulikuwa unazuia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu.

Serikali mpya rais Bola Tinubu, iliondoa mpango huo kwa misingi kuwa ulikuwa unachukua sehemu kubwa ya fedha za serikali.

Mamlaka kwenye taifa hilo ilisema pesa zilizokuwa zinatumika kuweka ruzuku kwa bidhaa za mafuta ziingetumika katika miradi mingine ya serikali.

Vyama hivyo sasa vinatoa wito kwa serikali kuongeza malipo ya kila mwezi kufikia angalau Dolla za Marekani 120 kutoka kwa Dolla 36.

Rais wa chama cha wafanyikazi cha TUC Festus Osifo katika taarifa yake amesisitiza kuwa mgomo huo utaendelea hadi pale ambapo serikali itawajibika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live