Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Tinubu awalilia 25 waliofariki ajali ya lori

Ajali Lori Nigeria (600 X 307) Nigeria: Tinubu awalilia 25 waliofariki ajali ya lori

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Abiria 25 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 25 wamejeruhiwa baada ya roli lililokuwa limebeba vyakula kugongana na basi kusini mwa Nigeria, huku Rais wa nchi hiyo, Bola Tinubu akituma salamu za rambirambi.

Ajali hiyo ya imetokea jana Jumanne katika Kijiji cha Takalafia wilayani Magama, ambapo lori hilo imeelezwa lilikuwa linakwenda Lagos mji mkuu wa Nigeria.

Kiongozi wa kiserikali wa wilaya hiyo, Mohammed Umaru amesema majeruhi zaidi ya 25 walipelekwa hospitali na maiti zimehifadhiwa hospitalini, huku majeruhi wengine wakiruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupata matibabu.

Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni kuzidisha mizigo na abiria na mwendo wa kasi.

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu ametuma salamu za rambirambi na kuwataka wanananchi kufuata sheria za usalama barabarani katika kipindi hiki kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

“Rais Tinubu ameagiza majeruhi wapatiwe matibabu haraka na kwa usahihi ili waweze kurejea kwenye majukumu yao mbalimbali,” imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wa serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live