Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Serikali yaongeza mishahara kwa wafanyakazi

Rais Wa Nigeria Aagiza Maafisa Wa Usalama Kuokoa Wanafunzi Waliotekwa Nyara Nigeria: Serikali yaongeza mishahara kwa wafanyakazi

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nigeria imeongeza mishahara kwa watumishi wa umma kwa kati ya asilimia 25% na 35% huku ikiwasaidia kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha.

Mfanyakazi wa serikali anayelipwa mshahara mdogo zaidi sasa atapata Dola 324 sawa na shilingi Tsh. 839,160.84 kwa mwaka, shirika la habari la Reuters linaripoti.

Polisi na maafisa wa jeshi ni miongoni mwa wafanyakazi wa serikali ambao wanatarajiwa kufaidika na nyongeza ya mishahara, ambayo itarejeshwa hadi Januari.Tangazo hilo limekuja usiku wa siku ya wafanyakazi Jumatano.

Hata hivyo, kiwango cha mfumuko wa bei kwa sasa ni zaidi ya 30% - idadi kubwa zaidi katika karibu miongo mitatu ambapo gharama ya chakula imeongezeka hata zaidi - kwa 35%, kulingana na data ya hivi karibuni kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live