Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Ni miaka 10 sasa tangu kutekwa kwa wasichana wa shule 276

Nigeria Utekaji Miaka 10.png Nigeria: Ni miaka 10 sasa tangu kutekwa kwa wasichana wa shule 276

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Nigeria, imetia miaka 10 tangu kutekwa kwa wasichana wa shule 276 wa Chibok katika jimbo la Borno Kaskazini mwa Nigeria, na kundi la kigaidi la Boko Haram, baadhi ya wasichana hao, mpaka leo hawajapikana.

Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu yakiongozwa na Amnesty International, yanasema serikali ya Nigeria inapaswa kufanya jitihada za kuhakikisha kuwa wasichana karibu 100 ambao hawajapatikana baada ya kutekwa na Boko Haram, wanaunganishwa tena na familia zao.

Aidha, wanataka ulinzi kuimarushwa kwenye shule hasa Kaskazini mwa Nigeria, ili kuzuia utekwaji wa watoto hasa wanafunzi, jambo ambalo limekuwa likiendelea mara kwa mara tangu sakata la wasichana wa Chibok.

Kwa wazazi ambao hawajawaona wasichana wao, kama Yana Galang, kila siku ni huzuni kwao. Anaishi na matumaini kuwa siku moja, binti yake atapatikana na kurejea nyumbani.

Utekaji wa wanafunzi hao ulishtumiwa na kulaaniwa kote duniani, huku serikali ya Nigeria ikiahidi kuwaokoa wanafunzi hao na kulitokomeza kundi la Boko Haram, lakini miaka 10 baadaye hali imeendelea kuwa mbaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live