Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria, Morocco kufadhili bomba refu zaidi la gesi baharini duniani

Gesi Urusii.jpeg Nigeria, Morocco kufadhili bomba refu zaidi la gesi baharini duniani

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nigeria na Morocco zitawekeza dola bilioni 12.5 kila moja katika bomba la gesi linalounganisha nchi hizo mbili na kupitia mataifa 11 ya Afrika Magharibi. Likiwa na takriban kilomita 5,600, bomba hilo linatarajiwa kuweka rekodi ya kuwa bomba refu zaidi la gesi baharini duniani.

Kampuni ya Kitaifa ya Petroli ya Nigeria (NNPCL) na Ofisi ya Kitaifa ya Hidrokaboni na Migodi ya Morocco (ONHYM) zinatazamiwa kufadhili kwa pamoja bomba la gesi kati ya Nigeria na Morocco la dola bilioni 25 kwa hisa sawa.

Mallam Mele Kyari, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kitaifa ya Petroli ya Nigeria, amesema kuwa mradi huo tayari uko katika Awamu ya Pili ya utafiti wa awali na kwa sasa unafanyiwa tathmini ya athari za mazingira – pamoja na uchunguzi wa haki za njia.

Kyari amesema Kampuni ya Kitaifa ya Petroli ya Nigeria inatumia hifadhi kubwa ya gesi asilia ya Nigeria, ambayo inajumuisha zaidi ya mita za ujazo bilioni 5,6. Amesema hifadhi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia karibu mita za ujazo bilioni 17.

Amesema kuwa hifadhi hiyo kubwa itapelekea kustawi sekta za nishati na viwanda. Kyari pia amesisitiza kuwa gesi itasaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na kupambana na ukosefu wa ajira na umaskini.

Kwa mujibu wa mpango uliopo wa mradi huo, bomba hilo litapita katika mwambao wa Afrika Magharibi kutoka Nigeria, kupitia Benin, Togo, Ghana, Côte d'Ivoire, Liberia, Sierra Leone, Guinea, Guinea-Bissau, Gambia, Senegal na Mauritania hadi Morocco.

Pia bomba hilo linatazamiwa kufikishwa katika nchi zisizo na mipaka ya baharini za Niger, Burkina Faso na Mali. Hatimaye bomba hilo la gesi kutoka Nigeria litaunganishwa kwenye bomba la gesi la Morocco-Ulaya na hivyo kuunganishwa na mtandao wa gesi wa Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live