Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Mkuu wa kanisa la Methodist atekwa

Methodist Mkuu Nigeria Mkuu wa kanisa la Methodist atekwa

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Kanisa la Methodist nchini Nigeria, Samuel Kanu, ametekwa nyara pamoja na makasisi wengine wawili walipokuwa wakirejea kutoka kwa shughuli za la kanisa.

Watu hao walikuwa wakisafiri kwenye barabara kuu siku ya Jumapili katika jimbo la kusini-mashariki la Abia walipotekwa nyara, polisi wa eneo hilo waliambia BBC.

Haijabainika ni nani aliyehusika, lakini vikundi vya wanaotaka kujitenga mara kwa mara hufanya utekaji nyara katika eneo hilo.

Polisi wanasema wameanzisha shughuli yai ya uokoaji kuwatafuta makasisi hao.

Utekaji nyara, mara nyingi kwa ajili ya fidia, ni jambo la kawaida katika sehemu nyingi za Nigeria.

Kumekuwa na ongezeko la mashambulio kutoka kwa magenge yenye silaha yakiwemo makundi ya wanamgambo wa kijihadi wakati Nigeria inapojiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Pia kumezuka kuzuka kwa mashambulizi ya magenge yenye silaha, yakiwemo makundi ya wapiganaji wa Kiislamu kaskazini mwa nchi hiyo, huku nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Hivi majuzi, mbunge wa eneo hilo alitekwa nyara na watu wasiojulikana. Mwili wake usio na kichwa ulipatikana siku chache baadaye.

Wanandoa wa kijeshi pia walikatwa vichwa walipokuwa wakisafiri kwenda eneo hilo kuwajulisha jamaa zao kuhusu mipango yao ya kufunga ndoa.

Kando Jumapili asubuhi, mwanamke mchanga na kaka yake walitekwa nyara wakati watu wenye silaha walipovamia makazi yao huko Lafia, jimbo la Nassarawa, karibu na mji mkuu, Abuja.

Baba yao hakuuawa wakati wa shambulio hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live