Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Mauaji ya Wapalestina Gaza hayahalalishiki

Zaidi Ya Watu 30,000 Wameuawa Gaza, Hamas Wasema Nigeria: Mauaji ya Wapalestina Gaza hayahalalishiki

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria amesema vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza haviwezi kuhalalalishika kwa njia yoyote ile.

Yusuf Tuggar amesema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya al-Jazeera na kuongeza kuwa, "Vita hivi vinapasa kusimamishwa mara moja. Hakuna kitu kinachoweza kuhalalisha utumiaji wa nguvu kupita kiasi dhidi ya wanawake, watoto na vichanga visivivyo na hatia Gaza.

Huku akikosoa undumakuwili wa Wamagharibi kuhusiana na vita hivyo, mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Nigeria amesema Abuja inaunga mkono uundwaji wa madola mawili kama suluhu ya mgogoro wa Palestina na kusisitiza kuwa, Palestina ina kila haki ya kuwa na mamlaka ya kujitawala na kuunda taifa huru.

"Dunia inapasa kuacha undumakuwili kuhisiana na mauaji yanayoendelea katika ukanda uliozongira wa wa Gaza," ameongeza Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Nigeria katika mahojiano na al-Jazeera.

Haya yanajiri siku chache baada ya Jeje Odongo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda kusema anasikitishwa sana na kushindwa jamii ya kimataifa katika kutatua mgogoro wa Gaza wakati huu ambapo utawala haramu wa Israel unatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo.

Hadi sasa vita hivyo vya mauaji ya kimbari vimepelekea kuuawa Wapalestina zaidi 30,500, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huku wengine zaidi 72,000 wakijeruhiwa.

Afrika Kusini ni katika nchi za Afrika ambazo zimekuwa mstari wa mbele kulaani vita hivyo vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023. Mwishoni mwa 2023, nchi hiyo ilifungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, ikiituhumu Israel kwa mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Gaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live