Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Jengo laporomoka, makumi wajeruhiwa

Gorofa Nigeria: Jengo laporomoka, makumi wajeruhiwa

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashirika ya dharura yanasema juhudi zinaendelea kuokoa idadi isiyojulikana ya watu waliokwama katika jengo lililoanguka siku ya Alhamisi katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Jengo hilo la ghorofa tatu, ambalo lilikuwa likijengwa, liko Gwarinpa, kitongoji cha makazi.

Nkechi Isa, msemaji wa Shirika la Usimamizi wa Wilaya ya Mji Mkuu wa Shirikisho, alisema katika taarifa kwamba watu wasiopungua 19 hadi sasa wameokolewa huku mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya.

Alisema waathirika hao, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa ujenzi, wamepelekwa katika hospitali zinazozunguka katikati ya jiji.

Timu ya pamoja ya vyombo vya dharura na usalama ilikwenda eneo la tukio kusaidia katika uokoaji. Baadhi ya kampuni za ujenzi zenye vifaa vizito  pia zimeingia kusaidia katika juhudi za uokoaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live