Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger yatangaza siku tatu za maombolezi baada ya kuuliwa wanajeshi wake 29

Niger Yatangaza Siku Tatu Za Maombolezi Baada Ya Kuuliwa Wanajeshi Wake 29 Niger yatangaza siku tatu za maombolezi baada ya kuuliwa wanajeshi wake 29

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Voa

Wanajeshi 29 wa Niger wameuliwa kufuatia shambulio la kigaidi magharibi mwa nchi, ikiwa ni idadi kubwa ya watu kuuliwa tangu wanajeshi kuchukua madaraka ya taifa hilo mwezi Julai.

Wizara ya ulinzi ilitangaza mauwaji hayo jumatatu usiku ikieleza kwamba kundi la wanajeshi wa usalama lilishambuliwa kaskazini magharibi mwa Tabatol, kwa kutumia mchanganyiko wa silaha ikiwa ni pamoja na vilipuzi na magari yaliyoendesha na karibu magaidi 100 walojitoa mhanga.

Wanajeshi wawili wamejeruhiwa vibaya na darzeni kadhaa ya magaidi waliuliwa.

Shambulio lilitokea karibu na mpaka wa Mali, wakati wa operesheni ya kijeshi iliyokua na lengo la kukabiliana na kuzia shambulio hilo lililofanywa na kundi la Islamic State katika eneo hilo kulingana na taarifa ya wizara.

Wizara ya ulinzi inasema mawasiliano kutoka magaidi walolazimika kukimbia yalinaswa, na kwamba washambuliaji walipata msaada kutoka waatalamu wa nje bila ya kutoa maelezo zaidi.

Taarifa imesema wanajeshi wamefariki kama mashuja na siku tatu za maombolezi ya kitaifa zimetangazwa.

Uwasi unaoendeshwa na wanamgambo wa kislamu umekumba kanda ya Sahel, magharibi ya Afrika kwa zaidi ya muongo mmoja, ukianzia kaskazini mwa Mali mwaka 2012 kabla ya kusamba katika nchi jirani za Niger na Burkina Faso mwaka 2015.

Mwezi Ogusti karibu wanajeshi 17 wa Niger waliuliwa na 20 kujeruhiwa katika shambulio linalodhaniwa lilifanywa na wanamgambo karibu na mpaka wa Niger na Burkina Faso.

Chanzo: Voa