Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger yasimamishwa na Umoja wa Afrika baada ya mapinduzi

Niger Yasimamishwa Na Umoja Wa Afrika Baada Ya Mapinduzi Niger yasimamishwa na Umoja wa Afrika baada ya mapinduzi

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Umoja wa Afrika (AU) umeisimamisha Niger kutoka kwa shughuli zake zote baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi uliopita.

Baraza la Amani na Usalama la AU lilitoa wito kwa nchi zote wanachama wake na jumuiya ya kimataifa kujiepusha na hatua zozote zinazoweza kuhalalisha utawala wa kijeshi nchini Niger.

Ulikariri wito kwa viongozi wa mapinduzi kumwachilia huru Rais mteule Mohamed Bazoum.

Umoja wa ukanda wa Afrika Magharibi, Ecowas tayari imetishia hatua za kijeshi kumrejesha kazini.

Serikali ya Niger imesema kuwa utawala wa kiraia hauwezi kurejeshwa mpaka baada ya miaka mitatu, lakini hili limepuuzwa na Ecowas kuwa halikubaliki.

Chanzo: Bbc