Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger yamtaka Balozi wa UN aondoke nchini humo ndani ya saa 72

Niger Yatangaza Siku Tatu Za Maombolezi Baada Ya Kuuliwa Wanajeshi Wake 29 Niger yamtaka Balozi wa UN aondoke nchini humo ndani ya saa 72

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la kijeshi linalotawala Niger limemtaka Balozi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kuondoka katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi katika kipindi cha saa 72 zijazo.

Baraza hilo linautuhumu Umoja wa Mataifa kuwa ulikula njama nyuma ya pazia na chini ya mashinikizo ya Ufaransa, iliyopelekea nchi hiyo ya Kiafrika inyimwe haki ya kushiriki kikamilifu katika mkutano wa Baraza Kuu la umoja huo mwezi uliopita mjini New York.

Serikali ya Paris hadi hivi sasa inakataa kuitambua serikali iliyoundwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi, na hapo awali ilikaidi amri ya jeshi hilo ya kuondoa balozi na wanajeshi wa Ufaransa nchini humo ikidai kuwa, amri hiyo ilitoka kwa serikali isiyoitambua.

Hata hivyo Ufaransa hapo jana ilianza zoezi la kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger, baada ya kutimuliwa na baraza la kijeshi linalotawala nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kanali ya France 24 ilimnukuu msemaji wa Kamanda Mkuu wa jeshi la Ufaransa akisema kuwa, "Wanajeshi wetu ambao ni sehemu ya kikosi cha askari 1,400 wameanza kuondoka Niger Jumanne, huku wakisindikizwa na vikosi vya Niger." Kuondoka wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger

Wanajeshi hao wa Ufaransa waliofukuzwa kwa madhila nchini Niger wameelekea katika nchi nyingine ya Kiafrika ya Chad. Uhusiano wa Niger na Ufaransa pamoja na nchi nyingine za Magharibi uliharibika miezi miwili iliyopita, baada ya jeshi kumpindua rais ambaye wananchi wa Niger walikuwa wanalalamika vikali kwamba ni kibaraka mkubwa wa Ufaransa, Mohammad Bazoum.

Mwishoni mwa mwezi uliopita wa Septemba, maelfu ya wananci wa Niger walimiminika mitaani kusherehekea kutimuliwa balozi wa mkoloni Mfaransa nchini mwao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live