Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger yakubali mpango wa Algeria wa kutatua mzozo wa ndani wa nchi hiyo

Mzozo Algeriaaa Niger yakubali mpango wa Algeria wa kutatua mzozo wa ndani wa nchi hiyo

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria ilimengaza kuwa, Niger imekubaliana na mpango wa Algiers wa kutatua mgogoro wa ndani wa nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imetangaza leo Jumatatu kwamba, baada ya Niger kukubaliana na mpango wa Algiers wa kutatua mgogoro wa ndani wa Niger, Rais wa Jamhuri ya Algeria, Abdelmadjid Tebboune, amemtuma Waziri wa Mambo ya Nje, Ahmed Attaf, haraka iwezekanavyo kwenda Niamey, mji mkuu wa Niger, ili kuandaa utangulizi wa kuanza mazungumzo kati ya pande zote za Niger.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria, kukubaliwa mpango wa nchi hiyo kunazidisha nafasi ya kufanikiwa suluhisho la kisiasa la mzozo wa Niger na kunatayarisha mazingira mazuri ambayo yatawezesha kukomeshwa mgogoro huo kwa njia ya amani, ambayo italinda maslahi ya Niger na eneo zima la Magharibi mwa Afrika.

Itakumbukwa kuwa, tarehe 26 Julai 2023, Kikosi cha Gadi ya Rais wa Niger kilimuondoa madarakani rais wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum, kwa tuhuma za ufisadi, kushirikiana na nchi za Magharibi, na kutojali hali ya umaskini nchini humo.

Baada ya mapinduzi hayo, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilitishia kuingilia kijeshi kwa ajili eti ya kurejesha utawala wa sheria nchini Niger.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live