Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger yafungua tena mipaka yake baada ya mapinduzi ya Julai

Niqer Tishio Nigeria.jpeg Niger yafungua tena mipaka yake baada ya mapinduzi ya Julai

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafisa wa serikali ya kijeshi inayoongoza Niger wametangaza kuwa wamefungua tena anga ya nchi hiyo, ambayo ilikuwa imefungwa tangu tarehe 6 Agosti.

Msemaji wa Wizara ya Uchukuzi ya Niger ametangaza kwamba, viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo wamefungua tena anga ya nchi hiyo kwa safari zote za ndege.

Viongozi wa kijeshi wa Niger, ambao walichukua madaraka baada ya rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani mwezi Julai mwaka huu, walifunga anga ya Niger mnamo Agosti 6, 2023, kujibu tishio la mashambulizi ya kijeshi ya nchi jirani.

Maafisa wa baraza kuu la kijeshi la Niger wametangaza kwamba, anga ya nchi hiyo imefunguliwa tena kwa safari zote za ndege za ndani na nje ya nchi, lakini amri hiyo haijumuishi safari za ndege za kijeshi na "safari nyingine maalumu zinazohitaji idhini ya mamlaka husika".

Tarehe 26 Julai 2023, walinzi wa rais wa Niger walifanya mapinduzi dhidi ya rais wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum; na mkuu wa walinzi hao, Jenerali Abdourahamane Tchiani, alijitangaza kuwa kiongozi mpya wa nchi na mkuu wa baraza la mpito.

Sambamba na hayo wananchi wa Niger wameendelea kufanya maandamano mjini Niamey wakitaka kuondoka balozi wa Ufaransa na majeshi ya nchi hiyo katika ardhi na Niger.

Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya kijeshi ya Niger wiki iliyopita ilimpa balozi wa Ufaransa, Sylviin Yette, saa 48 kuondoka katika ardhi ya nchi hiyo.

Serikali ya kijeshi ya Niger ilitamka bayana kuwa balozi wa Paris hana tena upendeleo na kinga zinazohusiana na hadhi yake kama mfanyakazi wa kidiplomasia wa ubalozi wa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live