Kiongozi wa mapinduzi nchini Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, ametia saini amri inayoruhusu serikali za kijeshi za Mali na Burkina Faso kutuma wanajeshi wao nchini mwake kusaidia kujilinda dhidi ya shambulio.
Tangazo hilo lilitolewa baada ya mawaziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Olivia Rouamba na Mali, Abdoulaye Diop, kumtembelea Jenerali Tchiani mjini Niamey siku ya Alhamisi.
Muungano wa kanda ya Afrika Magharibi Ecowas umetishia kutumia nguvu kumrejesha madarakani rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia wa Niger, Mohamed Bazoum, ambaye aliondolewa madarakani na kundi la maafisa wa jeshi mwezi uliopita.
Ecowas imekuwa ikijaribu kufanya mazungumzo na viongozi wa mapinduzi lakini imeonya kuwa iko tayari kutuma wanajeshi ikiwa diplomasia itafeli.