Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger kulamba vikwazo EU?

Niqer Hali Tete.jpeg Niger kulamba vikwazo EU?

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Ulaya unajiandaa kuiwekea vikwazo serikali mpya ya kijeshi nchini Niger, duru za Ulaya ziliambia Reuters siku ya Jumatano.

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya na afisa mmoja aliyehusika katika kuunda vikwazo hivyo alithibitisha kuwa umoja huo ulikuwa unabuni vifurushi vya adhabu, vikihusisha "kudhoofisha demokrasia."

Mpango huo huenda ukakubaliwa, afisa huyo aliambia chombo cha habari.

"Hatua inayofuata itakuwa vikwazo dhidi ya wanachama binafsi wa serikali ya kijeshi, ambayo inasemekana kuhusika na kuondolewa kwa rais wa zamani Mohamed Bazoum mwezi uliopita," mwanadiplomasia huyo alisema.

Hakuna tarehe ambayo imetolewa ni lini vikwazo hivi vinaweza kutekelezwa, ingawa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 27 za umoja huo wanatarajiwa kujadili uwezekano wa vikwazo pamoja na masuala mengine yanayohusiana na Niger watakapokutana Toledo mnamo Agosti 31.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: