Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger imepiga marufuku uuzaji nafaka nje ya nchi

Urusi Iko Tayari Kurudi Kwenye Makubaliano Ya Nafaka Kwa Masharti Niger imepiga marufuku uuzaji nafaka nje ya nchi

Fri, 18 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utawala wa kijeshi wa Niger umepiga marufuku uuzaji nje wa mchele na nafaka kwa minajili ya kulinda bidhaa katika masoko yake ya ndani, isipokuwa kwa majirani zake wawili na washirika, Burkina Faso na Mali, serikali imetangaza.

Hatua hii "imeamuliwa na Jenerali Abdourahamane Tiani", mkuu wa mamlaka ya kijeshi, "ili kulinda usambazaji wa soko la ndani" na "kufanya bidhaa za matumizi kupatikana", inabainisha serikali katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumatano.

Katika orodha ya bidhaa zilizokumbwa na marufuku hii ya kuuza nje, kuna hasa mchele (unaozalishwa ndani ya nchi kwenye kingo za Mto Niger), ulezi na mtama (nafaka), kunde (aina ya maharagwe) na hata mahindi. "Marufuku haya hayatumiki kwa mauzo ya nje kwenda" Mali na Burkina Faso, majirani wawili pia wanaotawaliwa na viongozi wa mapinduzi ya kijeshi ambao wanaunda shirikisho la Muungano wa Nchi za Sahel (AES) na Niger, inabainisha mamlaka . Vikwazo vya uhalifu vinaweza kuchukuliwa dhidi ya watu watakaokiuka sheria hii, na mizigo inaweza kukamatwa, taarifa ya inaoongeza.

Niger ni chanzo muhimu cha usambazaji wa nafaka, haswa kwa baadhi ya majimbo katika nchi jirani ya Nigeria. Ingawa vikwazo viliondolewa mwezi Februari, vikwazo vilivyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) dhidi ya Niger, baada ya mapinduzi yaliyomweka Jenerali Tiani madarakani mwezi wa Julai 2023, vimevuruga pakubwa usambazaji wa mara kwa mara katika masoko ya Niger ambako bado kuna mfumuko mkubwa wa bei kwenye baadhi ya bidhaa kama vile mchele.

Kuendelea kufungwa kwa mpaka na nchi jirani ya Benin kunachangia usumbufu huu. Mwaka huu, Wizara ya Kilimo imeahidi kuwanunulia wakulima sehemu ya mavuno yao, ambayo yatarejeshwa kwenye hifadhi ya chakula nchini.

Lakini pamoja na mafuriko makubwa ambayo yameikumba nchi nzima, wizara ina matumaini ya "mavuno mazuri ya kilimo". Takriban watu milioni moja na nusu wameathiriwa na mvua ya kipekee iliyonyesha nchini Niger na kusababisha vifo vya watu 339, kulingana na takwimu rasmi.

Mamlaka ya Niamey pia iliamua wiki hii kupunguza bei ya saruji kwa asilimia 35 ili kuruhusu wakazi kujijenga upya baada ya uharibifu uliosababishwa na mafuriko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live