Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger: Utawala wa kijeshi wamwachia huru mwana wa kiume Mohamed Bazoum

Niger: Utawala Wa Kijeshi Wamwachia Huru Mwana Wa Kiume Mohamed Bazoum Niger: Utawala wa kijeshi wamwachia huru mwana wa kiume Mohamed Bazoum

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Mtoto wa kiume wa Rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum ameachiliwa huru na mahakama ya kijeshi baada ya kukaa kizuizini kwa zaidi ya miezi mitano.

Salem Bazoum aliondoka kuelekea Togo baada ya juhudi za upatanishi za viongozi wa eneo hilo kukusaidia kuachiwa kwake.

Alizuiliwa pamoja na wazazi wake katika ikulu ya rais baada ya jeshi kufanya mapinduzi Julai mwaka jana.

Wazazi wake bado wako kizuizini, huku jutawala wa kijeshi ikikataa kuitikia shinikizo la kidiplomasia kuwaachilia.

Katika taarifa, mahakama ya kijeshi ilisema kuwa kuachiliwa kwa Bw Bazoum Jnr ni kwa muda tu, na "tutawasilaian naye mara tu atakapohitajika kufanya hivyo".

Alikuwa ameshtakiwa kwa njama ya kuhujumu mamlaka ya serikali kufuatia mapinduzi hayo.

Mnamo Oktoba, junta ilidai kuwa rais aliyepinduliwa na familia yake, wapishi wake wawili na maafisa wawili wa usalama walifanya jaribio lisilofaulu la kutoroka.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo Robert Dussey alikuja Niger kumsindikiza Bw Bazoum Jnr nje ya nchi, taarifa ya mahakama hiyo ilisema. Serikali ya Togo ilithibitisha kuachiliwa kwake, lakini haikutoa maelezo kuhusu aliko.

Sierra Leone pia ilihusika katika juhudi za upatanishi ili kupata kuachiliwa kwa mtoto wa kiume wa rais aliyepinduliwa, iliongeza katika taarifa yake.

Mwezi uliopita, mahakama ya muungano wa kanda ya Afrika Magharibi Ecowas iliamua kwamba kuzuiliwa kwa familia ya Bazoum ilikuwa hatua ya kiholela.

Iliamuru kuachiwa kwao, na kurejeshwa kwa Bw Bazoum kama rais.

Utawala wa kijeshi umepuuza uamuzi huo, na umesema kuwa kutakuwa na mpito wa hadi miaka mitatu kwa utawala wa kiraia.

Bw Bazoum aliondolewa madarakani na mkuu wa walinzi wa rais, Jenerali Abdourahamane Tiani, katika mapinduzi ambayo yalilaaniwa na Ecowas na mataifa ya Magharibi, ikiwa ni pamoja na ukoloni wa zamani Ufaransa.

Chanzo: Bbc