Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger: Mashirika ya ndege yagoma kuwabeba wafaransa

Mashirika Ndegegegege.png Niger: Mashirika ya ndege yagoma kuwabeba wafaransa

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashirika ya ndege yanayofanya safari kwenda Niamey, mji mkuu wa Niger, yameamua kutochukua tena abiria wa Ufaransa kwenda eneo hili, shirika la habari la AFP limebaini likinukuu vyanzo vya uwanja wa ndege siku ya Jumatano.

"Kulingana na mamlaka ya Niger, abiria yeyote mwenye uraia wa Ufaransa hana idhini tena ya kuingia tena kwenye ardhi ya Niger, kwa hivyo hatakubaliwa tena kwenye safari zetu za ndege kuelekea nchi hii," inaonyesha memo ya ndani ya Air Burkina ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi.

"Abiria wa Ufaransa wanaoelekea Niamey hawawezi tena kupanda" ndege za Royal Air Maroc (RAM), "bila idhini maalum kutoka kwa mamlaka ya Niger na wamekuwa wakifanya hivyo kwa karibu wiki, moja" kulingana na chanzo kilicho karibu na kampuni.

Makampuni mengine yanayofanya safari kenda Niamey, kama vile Ethiopian Airlines, Asky, Air Tunisie na Turkish Airlines, awali hawakujibu swali la iwapo wataendelea kuwapeleka raia wa Ufaransa nchini Niger.

Pia ikihojiwa, mamlaka ya Niger bado haijathibitisha kwamba Wafaransa wanaotaka au kulazimika kuja Niamey sasa wamepigwa marufuku kungia kwenye ardhi yaNiger. Watu kadhaa wa Ufaransa walifukuzwa hivi majuzi walipowasili katika uwanja wa ndege wa Niamey, kulingana na vyanzo vya uwanja wa ndege.

Uhusiano kati ya Ufaransa na Niger umeendelea kuzorota tangu mapinduzi ya kijeshi ya Julai 26, 2022 yaliyompindua rais mteule Mohamed Bazoum. Ubalozi wa Ufaransa nchini Niger, ambao Paris ilitangaza kufungwa muda mfupi kabla ya Krismasi, umefungwa rasmi na utaendelea na shughuli zake kutoka Paris, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ilitangaza siku ya Jumanne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live