Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger, Mali na Burkina Faso kuunda kikosi cha pamoja ili kupambana na wanajihadi

Niger, Mali Na Burkina Faso Kuunda Kikosi Cha Pamoja Ili Kupambana Na Wanajihadi Niger, Mali na Burkina Faso kuunda kikosi cha pamoja ili kupambana na wanajihadi

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Niger, Mali na Burkina Faso wanasema wataunda kikosi cha pamoja ili kupambana na vitisho vya wanajihadi katika nchi zao.

Mkuu wa jeshi la Niger Moussa Salaou Barmou alitangaza kuwa kitaanza kazi haraka iwezekanavyo, bila kutoa maelezo ya ukubwa wake.

Alizungumza katika hotuba ya televisheni siku ya Jumatano kufuatia mazungumzo katika mji mkuu Niamey.

Makundi yenye uhusiano na Islamic State na al-Qaeda yameua maelfu ya watu katika eneo hilo katika mwaka uliopita.

Tawala za kijeshi katika nchi hizo tatu zimezidi kuwa washirika wa karibu katika miezi ya hivi karibuni.

Septemba iliyopita, waliunda mkataba wa ulinzi wa pande zote unaojulikana kama Muungano wa Mataifa ya Sahel, wakijiondoa kutoka kwa kikosi cha kimataifa, G5, kilichoundwa kupambana na makundi ya jihadi katika eneo hilo.

Ghasia katika eneo la Sahel la Afrika Magharibi zimezidi kuwa mbaya katika miaka ya hivi karibuni licha ya ahadi za serikali za kijeshi kukabiliana na mzozo wa muongo mmoja na makundi ya kijihadi.

Nchi hizo tatu zote zimekatiza uhusiano wao na Ufaransa, ukoloni wa zamani, ambao kwa miaka mingi ulikuwa na uwepo mkubwa wa kijeshi katika eneo la Sahel.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali, Minusma, ambao ulikuwa umekuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja pia uliamriwa na viongozi wa nchi hiyo kujiondoa "bila kuchelewa", na kukamilisha kuondoka mwezi Desemba.

Tawala za kijeshi zimeimarisha uhusiano na Urusi, ambayo imeingia kuziba pengo.

Pia wametangaza kuwa wanaondoka katika jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi Ecowas.

Chanzo: Bbc