Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niger: Mahakama yaagiza kuachiliwa kwa muda kwa mawaziri wanne wa zamani

HUKUMU Niger: Mahakama yaagiza kuachiliwa kwa muda kwa mawaziri wanne wa zamani

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Niger, Mahakama ya Rufaa ya Niamey siku ya Jumatatu Julai 29 imeagiza kuachiliwa kwa muda kwa mawaziri wanne wa zamani kutoka kwa utawala uliopinduliwa wa rais wa zamani Mohamed Bazoum. Wakishtakiwa kwa "kuhatarisha usalama wa taifa" na "uhalifu wa uhaini", sasa wanasubiri amri ya kuondoa kifungo chao ili waachiliwe rasmi.

Nchini Niger, Jumatatu jioni, mawaziri wanne wa zamani wa utawala uliopinduliwa wa rais wa zamani Mohamed Bazoum walipokea notisi ya mahakama iliyoagiza kuachiliwa kwao kwa muda. Kwa sasa bado wanasubiri amri ya kuwaondoa kifungoni ili kurejesha uhuru wao rasmi.

Mawaziri hao wa zamani waliokamatwa siku moja baada ya mapinduzi ya Julai 26, 2023, wanashitakiwa kwa "kuhatarisha usalama wa taifa" na "kosa la uhaini".

Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Hama Amadou Souley, Waziri wa zamani wa Fedha Ahmat Jidoud, Waziri wa zamani wa Nishati Ibrahim Yacoubou, na Waziri wa zamani wa Mipango Rabiou Abdou walitumia zaidi ya mwaka mmoja kizuizini. Kulingana na wakili wao, kosa lao pekee ni kulaani hadharani mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Baraza la Kitaifa la Kulinda Nchi ya Baba (CNSP) au kuchukua nafasi za uwajibikaji wakati wa tukio.

Hakuna lawama kutoka kwa mtazamo wa jinai kwa MaƮtre Illo Issoufou, mmoja wa mawakili wa washtakiwa, ambaye anashutumu kesi iliyo tupu dhidi ya wateja wake. Alipohojiwa kwa njia ya simu, amekaribisha tangazo la kuachiliwa kwao kwa muda wakati wa kusikilizwa kwa kesi katika Mahakama ya Rufaa ya Niamey. Anatangaza "kuendelea kupambana ili wafungwa wengine waachiliwe".

Takriban wafungwa ishirini wa kisiasa walio karibu na serikali iliyoondolewa bado wako kizuizini

Wafungwa zaidi ya ishirini wa kisiasa walio karibu na utawala ulioondolewa bado wako kizuizini. Miongoni mwao ni kiongozi wa kihistoria Abba Sani Issoufou, Waziri wa zamani wa Mafuta na mtoto wa Rais wa zamani Mahamadou Issoufou, anayezuiliwa katika gereza lililo kilomita 180 kutoka mji mkuu, Niamey.

Hatimaye, Mohamed Bazoum bado anashikiliwa katika sehemu za ikulu ya rais tangu mapinduzi ya kijeshi mwaka mmoja uliopita. Anakataa kujiuzulu wadhifa wake kama rais wa Jamhuri, licha ya shinikizo kutoka kwa wanajeshi walio madarakani. Katikati ya mwezi wa Julai, mahakama ya serikali iliondoa kinga ya mkuu wa nchi aliyeondolewa madarakani. Uchunguzi wa "kuhatarisha usalama wa taifa" na "uhalifu wa uhaini" bado unaendelea na kesi inaweza kusikilizwa katika wiki au miezi ijayo, na washtakiwa wote kusikilizwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live