Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nguvu haiwezi kutatua mgogoro wa Rwanda na Congo - Kagame

Paul  Kagame.jfif Nguvu haiwezi kutatua mgogoro wa Rwanda na Congo - Kagame

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ametoa wito wa kutatuliwa kwa mgogoro wa kisiasa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika mahojiano na shirika la utangazaji la serikali, alisema uhasama uliopo hauwezi kutatuliwa kwa nguvu pekee.

Wiki mbili zilizopita viongozi wa Afrika Mashariki waliidhinisha kuundwa kwa kikosi cha kijeshi cha kanda katika eneo lenye machafuko, huku kukiwa na kuzuka upya kwa shughuli za waasi na kuzidisha mvutano kati ya DR Congo na Rwanda.

Kigali inaishutumu serikali ya Congo kwa kulivamia eneo lake.

Kinshasa inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23. Kuhusu mpango wa wahamiaji na Uingereza, Rais Kagame alisema nchi hiyo ina nafasi kwa Wanyarwanda pamoja na mataifa mengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live