Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngunyi adai Ruto na Raila kuungana ni pigo kwa Mt Kenya

Ngunyi Adai Ruto Na Raila Kuungana Ni Pigo Kwa Mt Kenya Ngunyi adai Ruto na Raila kuungana ni pigo kwa Mt Kenya

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mchambuzi na mchanganuzi wa masuala na sera za kisiasa msomi Mutahi Ngunyi anahisi kwamba endapo Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga watafanikiwa kupatana kwa mazungumzo, basi wahasiriwa wakubwa watakuwa watu wa kutoka Mlima Kenya.

Ngunyi kupitia ukurasa wake wa Twitter alizua kwamba kuna dalili zote za wawili hao kupatana hivi karibuni kufuatia juhudi za kamati ya mazungumzo ya kitaifa, NADCO na hilo likifanikiwa, basi watu wa Mlima Kenya wajue ndio mwisho wao kukaa karibu na uongozi wa kipindi cha karne moja ijayo.

Ngunyi alisema kwamba Ruto ni mtu makini sana katika siasa na analenga kutia kikapuni kura zote za Magharibi mwa Kenya – eneo ambalo ni la pili kwa wingi wa kura na linahesabika kama ngome ya Bwana Odinga.

“Wakikuyu wapendwa: JAMII ya Mulembe ni ngome ya pili kwa ukubwa na wingi wa kura nchini Kenya. Naye Ruto atarekebisha uzio na Raila. Wakija PAMOJA, mtakuwa nje ya serikali kwa miaka 100,” Ngunyi alisema.

Msomi huyo wa kisiasa aliwataka watu wa Mlima Kenya kujiweka tayari kukubali matokeo lakini pia akawataka wasimchukie Ruto kwani wakianza kumuonesha chuki ndio mwisho wao kabisa kukaribishwa karibu na uongozi kama ambavyo sasa hivi wamekaribishwa.

“Kuwa wema kwa Ruto. Amekuwa mzuri kwenu. Ichukue AU iache. Mwisho u karibu!” alimaliza.

Itakumbukwa Ngunyi alikuwa anapinga sana sera za Ruto na kutetea muungano wa Uhuru Kenyatta na Raila Odinga lakini mwaka mmoja baada ya Ruto kuwa rais, Ngunyi alijirekebisha na kurudi upande wa serikali ambapo amekuwa akitoa kauli za kutetea uongozi wa Kenya Kwanza.

Katika tweet nyingine, Ngunyi alisisitiza kwamba Ruto hakuna mahali ataenda kabla ya kumaliza miaka 10 katika uongozi kama rais.

“RUTO LAZIMA AENDE. Aenda wapi? Hii ni CHINI kadri anavyoweza kwenda. Kuanzia hapa, anaweza tu KUPANDA. Na "JUU" atakwenda. Hakuna SHULE ya Urais (JF Kennedy). Unajifunza kazini. Na ikiwa mwaka wa kwanza sio wa kutetereka, HUJIFUNZI. Mpe NAFASI,” Ngunyi alisema.

Chanzo: Radio Jambo