Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngono zembe yaongeza kasi ya VVU kwa Vijana

GettyImages 590279757 9b886dbd225a485fb8d2e1a2c09ca484 Ngono zembe yaongeza kasi ya VVU kwa Vijana

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa taarifa ya Chuo Kikuu cha Hospitali ya Aga Khan cha jijini Nairobi, imebainika chanzo ni Watoto waliozaliwa na Maambukizi ambao sasa wamekuwa Vijana au Watu wazima na kujihusisha na Ngono bila kuchukua tahadhari

Dkt. Adeel Shah, Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza na Watoto kutoka #AgaKhan amesema "Vijana hawa na Watu Wazima wamekuwa Kundi la Maambukizi, wanaingia kwenye mahusiano na wenzao wasio na VVU na kushiriki Ngono bila kinga, hali inayowaweka Watu wengi zaidi katika Maambukizi"

Sababu nyingine ni Vijana waliogeuza Miili yao kama Kitega Uchumi kwa kujihusisha na Ngono na Watu wazima kwa lengo la kujipatia Fedha, matokeo yake wengi wameishia kupata Maambukizi ya VVU na Magonjwa mengine ya Zinaa kwasababu wanaokutana nao wanawapa masharti ya kutotumia Kinga.

Riipoti mpya ya Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI Nchini Kenya, imeonesha ongezeko la Watu 32,017 huku Vijana wakiwa 11,229 na wengi wao ni wenye umri wa Miaka kati ya 15 hadi 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live