Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngatia akutana na JSC, asema tajriba ya miaka 41 itafanya awe Jaji Mkuu bora

99f091ab72ecd88d Ngatia akutana na JSC, asema tajriba ya miaka 41 itafanya awe Jaji Mkuu bora

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Ngatia ana tajriba ya miaka 41 kama wakili na alisema tajriba yake itamsaidia kuendesha idara ya mahakama

- Alisema anajivunia kuwa alimaliza migomo ya Chuo Kikuu cha Nairobi baada ya seneti ya chuo hicho kumpa kibarua cha kutafuta suluhu la migomo hiyo

- Aliambia makamishna wasichague jaji mkuu mtarajiwa kwa msingi wa jinsia mbali akili za mtu kisheria

Wakili Fred Ngatia Jumanne Aprili 20 alifika mbele ya Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) kutafuta kazi ya Jaji Mkuu.

Ngatia atakuwa wa sabab kuhojiwa na JSC katika safari ya kumtafuta mrithi wa aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga.

Ngatia alifika kwenye mahojiano hayo katika Mahakama ya Upeo ambapo alikutana na makamishna wakiongozwa mwenyekiti Olive Mugenda akiwa amejihami na tajriba ya miaka 41.

Kulingana na wasifu wa Ngatia, aliorodheshwa kwenye sajili ya mawakili humu nchini mwaka wa 1980.

Ngatia alianza mahojiano kwa kuwamiminia sifa David Maraga na Willy Mutunga ambao alisema anawaenzi kwa kazi yao katika idara ya mahakama.

"Licha ya kuwa alitoka kwenye sekta ya mafunzo, Mutunga alifanya kazi kubwa ya mageuzi katika idara hii," alisema Ngatia

Ngatia alimulikwa pakubwa kuhusu uwezekano wake wa kuleta mageuzi kwenye idara hiyo iwapo atafanikiwa kupata kazi hiyo.

Kamishna Mohammed Warsame alimtia kwenye kikaango Ngatia kuhusiana na maamuzi ya mahakama ya upeo wakati wa kesi za matokeo ya uchaguzi wa urais 2013 na 2017.

"NIkipata hii nafasi ya kuwa Jaji Mkuu basi huo utakuwa ni mwisho wangu na Ngatia ambaye ni wakili. Nitafanya maamuzi yangu kwa mujibu wa sheria na katiba na wala si kwa mujibu ya nilivyokuwa nikiwakilisha wateja wangu awali," alisema Ngatia.

Wakili pia alichukua nafasi hiyo kuwajulisha Wakenya kuwa hayupo kwenye mitandao ya kijamii akisema yeye hupenda kuwa kwenye maktaba akisoma na kusema yeye hupata amani zaidi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke