Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Netflix yamaliza mpango wake wa usajili bila malipo nchini Kenya

Netflix Yamaliza Mpango Wake Wa Usajili Bila Malipo Nchini Kenya Netflix yamaliza mpango wake wa usajili bila malipo nchini Kenya

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya kutoa huduma za upeperushaji wa filamu Netflix imetangaza kuwa itasitisha huduma yake ya bure nchini Kenya mwezi ujao huku ikitafuta njia za kuongeza mapato yake huku kukiwa na ushindani wa soko.

Mnamo 2021, Netflix iliruhusu watumiaji katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kufikia baadhi ya filamu zake bila kulipia usajili.Hili lilikuwa jaribio la kuingia katika soko la Kenya linalokua.

Katika taarifa, Netflix inasema mpango huo wa bure hautapatikana tena kuanzia tarehe 1 Novemba.

"Hakuna hatua itakayohitajika, uanachama wako utaghairiwa moja kwa moja mpango wa bila malipo utakapokamilika," kampuni hiyo ilisema.

Iliwahimiza waliojisajili kuboresha hadi mipango mbalimbali ya malipo inayotolewa.

Hatua hiyo inajiri miezi kadhaa baada ya Netflix kupunguza bei ya usajili kwa wateja wake wa Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live