Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nestor Girukwishaka kiongozi mpya wa CNL

Nestor Girukwishaka 0JM Nestor Girukwishaka.

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nestor Girukwishaka ndiye ambaye amechaguliwa kuwa Kiongozi wa Chama cha CNL kwa muda wa miaka mitano akichukuwa nafasi ya Agathon Rwasa.

Ni baada ya kongamano ambalo limefanyikia mkoani Ngozi Kaskazini mwa Burundi likiongozwa na Mbunge Marie Immaculée Ntacobakimvuna akiwa miongoni mwa wabunge wanaompinga Agathon Rwasa.

Hata hivyo, upande wa wafuasi wa Agathon Rwasa, Mbunge Pamphile Malaika alisema kuwa mkutano huo haukubaliwi kisheria kwani anayeruhusiwa kuitisha ni Agathon Rwasa.

Baadhi ya wanachama kadhaa wa CNL walio upande wa Rwasa walikamatwa na kuitiwa nguvuni, wengine wakizuiwa kusafiri wapokuwa wanataka kushiriki katika kongamano lililoandaliwa na wapinzani wa Agathon Rwasa.

Kongamano hilo limefanyika mbunge Mhe.Agathon Rwasa akiwa nje katika safari ya kikazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live