Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndumbaro: Tanzania ndio Rais wa Cecafa

89470 Pic+cecafa Ndumbaro: Tanzania ndio Rais wa Cecafa

Sat, 21 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

NAIBU Waziri wa Mambo ya nje ya nchi, Damas Ndumbaro katika hutoba yake leo Jumamosi kwenye mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) amesema Tanzania ndio Rais wa Cecafa.

Akimpongeza raisi wa TFF, Wallace Karia kwa kuchaguliwa kwake kuiongoza Cecafa kumeiletea heshima Tanzania kuonekana ina mafanikio makubwa ya soka.

Amesema katika uongozi wake ndani ya miaka miwili amefanya mambo makubwa yanayofanya Tanzania ianze kutazamwa kwa jicho la kipekee.

"Kuchukua makombe nane ndani ya miaka miwili si jambo dogo, linastahili pongezi, lazima tukubali mabadiliko kuhakikisha tunafika mbali,"amesema. TENGA MWADILIFU Katika hotuba yake Ndumbalo amesema rais wa zamani wa TFF, Tenga ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kwamba ameacha alama kubwa katika uongozi wake.

Amesema ni vyema akapewa heshima yake akiwa hai kwa mabadiliko mengi ambayo aliyafanya kwenye uongozi wake.

"Kipindi cha nyumba kulikuwa hakuna uadilifu kwenye matumizi ya pesa lakini Tenga hakuwahi kuhusishwa na hilo,".

"Amebadilisha vitu vingi ndani ya TFF mfano katika mkutano kama huu ungeona makomandoo wengi kunapigwa ngumi hayo aliyaondoa kila kitu kinafanywa kwa amani,".

"Alianzisha Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo kwa sasa tunaona matunda yake, kuweka vitengo muhimu ndani ya TFF kafanya mengi anastahili pongezi," amesema.

Mbali na hilo pia amesema bila mabadiliko hakuna ambacho kitafanyika kwenye soka akitolea mfano wa enzi ya Mhidini Ndolanga Shirikisho liliitwa FAT na sasa TFF.

"Soka lazima liwe na mabadiliko kipindi cha Ndolanga ilikuwa FAT na sasa TFF, ndivyo inavyotakiwa kwenda na kasi ya sayansi na Tekinolojia,"amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz