Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu Wamuua Kaka Yako Kisa Amempiga Mama kwa Kachelewesha Chakula

Jeneza 3.jpeg Jeneza

Sat, 25 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndugu wawili ambao ni kaka na mdogo wake wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya kwa tuhuma za kumuua kaka yao mkubwa katika eneo la Elukhongo, Kaunti ndogo ya Butula.

Ndugu hao ambao ni, Pascaliano Odhiambo (29), na Bonventure Ouma (19) waliripotiwa kumshambulia kaka yao aitwaye Juma siku ya Jumatano, Septemba 22, baada ya kaka huyo kumpiga mama yao kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kucheleweshwa chakula.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Odhiambo na Ouma walimrukia mwenzao na kuanza kumchakaza baada ya kumkuta akimpiga mama yao aliyemwarifu chakula kilikuwa bado hakijaiva.

"Walimsikia mama yao akipiga mayowe na walipokimbia kujionea kilichokuwa kikiendelea, walimkuta Juma akimpiga. Walimrukia na kumpa kichapo cha mbwa kabla ya kwenda kulala," taarifa ya polisi ilisema.

Mnamo Alhamisi, majira ya saa 12 asubuhi, mama alienda katika nyumba yake Juma ili kumuangalia. Hata hivyo, alimkuta akiwa amekata roho kutokana na majeraha yaliyosababishwa na kipigo cha ndugu zake huku mwili wake ukiwa umelala mlangoni pake alikuwa na majeraha mabaya kichwani.

Mama huyo aliwaarifu viongozi wa eneo hilo waliotembelea eneo la tukio. Wapelelezi walikuta panga, jembe, na rungu inayoaminika kutumiwa na Ouma na Odhiambo kumuua ndugu yao.

Washukiwa hao walinaswa na kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Bumala wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live