Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndombele kuwa nje kwa mechi zilizosalia msimu huu

Ndombele Ndombele kuwa nje kwa mechi zilizosalia msimu huu

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Jose Mourinho amethibitisha kumkosa mchezaji wake Tanguy Ndombele kwa mechi zote mbili zilizobaki kumaliza msimu.

Ndombele aliumia goti walipokua mazoezini wakati Spurs ikijiandaa na michezo ya ligi inayoendelea hivi sasa.

Uthibitisho huo ulitolewa na Mourinho katika mahojiano yake na vyombo vya habari baada ya mchezo dhidi ya Newcastle ambapo Tottenham iliibuka na ushindi wa 3-1.

Ndombele raia wa Ufaransa amecheza jumla ya dakika 64 tu , tangu kurejea kwa msimu baada ya kusimama kutokana na tatizo la Corona pia inaelezwa hajawa na mahusiano mazuri na Kocha wake Jose Mourinho.

Awali kulikuwa na matumaini makubwa toka kwa mchezaji huyu ghali aliyelipiwa paundi milion 55 kama ada ya uhamisho toka Olympic lyon lakini tangu ametua Spurs hajakidhi mahitaji ya timu.

Tottenham iliyoko kwenye nafasi 7 katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 55 wamebakiza mechi mbili tu dhidi ya Leicester na Crystal Palace kumaliza msimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live