Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amewataka raia wake kuacha kukagua simu za wenza wao. Matamshi yake yalikuwa sehemu ya ombi la kujaribu kuzuia viwango vya talaka nchini humo.
Rekodi zinaonyesha nchi hiyo ilirekodi zaidi ya visa 22,000 vya talaka mwaka jana pekee, takwimu ambazo rais alizitaja kuwa za bahati mbaya.
Ukosefu wa haki za ndoa, uzinzi, unyanyasaji wa kijinsia, matusi na ukatili ni miongoni mwa sababu kubwa za watu waliotajwa mahakamani kutaka talaka.
"Tunafunga ndoa kwa ajili ya mapenzi, hatuoi kwenda kuangaliana, au kwenda kunyoosheana kidole," Bw Hichilema amenukuliwa na vyombo vya ndani .Takwimu za miezi 12 iliyopita zilionyesha ndoa fupi zaidi nchini ilidumu kwa siku 30 huku ndefu zaidi ikiwa ni miaka 65.