Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege zisizo na rubani zaharibiwa Mashariki mwa DRC

Drone Mashariki Tabbbb.png Ndege zisizo na rubani zaharibiwa Mashariki mwa DRC

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndege isiyo na rubani ya jeshi la Kongo ilishika moto siku ya Jumatano ilipokuwa inatua mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama na mamlaka ya uwanja wa ndege, huku ya pili ikidunguliwa na waasi wa M23 wiki mbili zilizopita.

Vyanzo vya usalama, mashahidi na wafanyakazi katika uwanja wa ndege wa Kavumba, ulioko karibu kilomita ishirini kaskazini mwa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, liliiambia AFP kuwa ndege isiyo na rubani aina ya CH-4 ya jeshi la DRC ilishika moto kwenye barabara ya kurukia ndege baada ya kugonga gari la zima moto kutoka RĂ©gie des. Voies Aires (RVA) wakati wa kutua kwake Jumatano asubuhi.

Maafisa wa RVA walisema baadhi ya wenzao walikamatwa kama sehemu ya uchunguzi, na wengine walijeruhiwa katika tukio hilo. Mwishoni mwa mwaka wa 2023, ndege tatu zisizo na rubani aina ya CH-4 zilizotengenezwa na China, zinazoendeshwa na kampuni ya kibinafsi inayoongozwa na watu wa Ufaransa, wakiwemo wanajeshi wa zamani, zilitumwa kwenye uwanja wa ndege wa Kavumba, kutoka ambapo zinapaa kwendakuanya mashambuizi dhidi ya waasi wa M23 na Jeshi la Rwanda katika maeneo yanayokaliwa na waasi katika mkoa jirani wa Kivu Kaskazini.

Mnamo Januari 8, vyanzo vya usalama vya ndani vya M23 vililiambia shirika la habari la AFP kwamba moja ya ndege zisizo na rubani ilidunguliwa asubuhi hiyo juu ya eneo linalodhibitiwa na waasi, bila kuweza kutaja eneo au mazingira. Siku ya Jumatano, katika video iliyochapishwa na kituo cha YouTube cha Sabyinyo News TV, chombo cha habari karibu na M23, Willy Ngoma, msemaji wa waasi hao, anabaini kile anachoelezea kama mabaki ya ndege isiyo na rubani ya CH-4 mali ya FARDC, majeshi ya DRC).

Mnamo Januari 17, waasi hao walitangaza kuwa makamanda wake wawili waliuawa katika shambulio ambalo, kulingana na vyanzo vya usalama, lilifanywa na ndege isiyo na rubani huko Kitshanga, takriban kilomita hamsini kaskazini mwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Maeneo mawili katika jimbo hili, Rutshuru na Masisi, yamekuwa katika mzozo tangu mwisho wa 2021 ambao unahusisha waasi wa M23, wanassaidiwa na jeshi la Rwanda, dhidi ya jeshi la Kongo, linalohusishwa na makundi yenye silaha na makampuni mawili ya jeshi la kigeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live