Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege zisizo na rubani za Iran zazinduliwa Nairobi

Dronesss (1).jpeg Ndege zisizo na rubani za Iran zazinduliwa Nairobi

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndege zisizo na rubani (drone) zinazozalishwa na makampuni ya teknolojia za kisasa nchini Iran zimezinduliwa katika Kituo cha Ubunifu na Teknolojia cha Jamhuri ya Kiislamu mjini Nairobi kwa madhumuni ya kuuzwa masokoni.

Kwa mujibu wa IRNA, ndege zisizo na rubani za kampuni zinazotumia maarifa za Iran, ambazo zina matumizi mawili ya "kunyunyizia" mashamba ya kilimo na pia "uimarishaji wa mashamba" na kubaini iwapo kuna wadudu waharibifu wa shambani, zimezinduliwa leo Jumatano wakati wa safari ya Rais Ebrahim Rais wa Jamhuri ya Kaiislamu ya Iran mjini Nairobi.

Droni hizo zimezinduliwa wakati Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alipotembelea Jumba la Ubunifu na Teknolojia la Iran (IHIT) mjini Nairobi kama sehemu ya safari yake nchini Kenya.

Ndege hiyo isiyo na rubani inayojulikana kama Pelikan 2 imetengenezwa na kampuni ya maarifa ya Iran, ambayo ina uwezo wa kipekee kama vile kuandaliwa kwa ajili ya kazi katika kipindi cha dakika 2, kunyunyizia hekta 2 katika kila oparesheni n.k.

Akiwa katika Jumba la Ubunifu na Teknolojia la Iran (IHIT) Rais wa Iran amesema jumba hilo ni moja ya vituo vinavyoongoza katika maendeleo ya uuzaji nje wa bidhaa zinazotokana na teknolojia mpya. Sayyid Ebrahim Raisi Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwa katika Jumba la Ubunifu na Teknolojia la Iran (IHIT) mjini Nairobi

Katika kituo hicho, zaidi ya kampuni 35 za teknolojia mpya za Iran zinazonesha na kusafirisha bidhaa zao nchini Kenya katika nyanja za dawa, vifaa vya matibabu, kilimo, ujenzi n.k.

Safari ya Rais Ebrahim Raisi nchini Kenya leo inatathminiwa kuwa na umuhimu mkubwa katika mabadilishano ya teknolojia na nchi hii ya Afrika Mashariki. Baada ya safari yake nchini Kenya, Rais Raisi ataekelea Uganda na kisha Zimbabwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live