Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege ya kijeshi yaanguka na kuwaka moto eneo la Oltinga kaunti ya Kajiado

C2c7c6d7ed5677bb Ndege ya kijeshi yaanguka na kuwaka moto eneo la Oltinga kaunti ya Kajiado

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ndege ya kijeshi aina ya chopa imeanguka eneo la Oltinga kaunti ya Kajiado na kulipuka motohata hivyo, haijabainika ni abiria wangapi walikuwemo.

Kamanda wa polisi kaunti ya Kajiado Muthuri Mwongera amesema ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa mbili asubuhi siku ya Alhamisi, Juni 24

Muthuri alisema ndege hiyo ililipuka moto baada ya kuangaka kilomita 60 kusini mwa eneo la Oloopolos.

" Nimemtuma OCPD wa Kajiado Magharibu Vincent Kitili kwenda eneo la tukio kule Oltinga ili atuletee habari zaidi kuhusu yaliyojiri," Muthuri alisema.

Muthuri pia alithibitisha kwamba ndege hiyo ilikuwa katika shughuli ya mafunzo na inahofiwa kuwa huenda abiria wote wameangamia.

Shughuli za uokoaji zinaendelea.

Mengi kukujuia...

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke