Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege ya KQ yalazimika kukatisha safari baada ya hitilafu

Ndege Ya KQ Yalazimika Kukatisha Safari Baada Ya Hitilafu Ndege ya KQ yalazimika kukatisha safari baada ya hitilafu

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Shirika la ndege nchini Kenya, KQ limeeleza kwamba ndege yake nambari KQ 310 imelazimika kurejea Nairobi baada ya kukumbwa na matatizo, ilikuwa na changamoto kwenye magurudumu yake.

Ndege hiyo iliyokuwa ikielekea jijini Dubai kutoka Nairobi,iliondoka uwanja wa ndege wa Jommo Kenyatta mwendo wa saa tatu usiku, ila maafisa wa uwanja wa ndege walipokuwa wakifanya shughuli zao , walikumbana na mabaki madogo ya gurudumu yalithibitishwa kutoka kwa ndege hiyo ambayo tayari ilikuwa angani.

Tarifa kuhusu hitilafu kwenye ndege hiyo zilianza kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya X na baadhi ya wanahabari nchini humo ambapo wakenya wengi walieleza hofu kubwa wakihoji kwamba ni kwa vipi hali ya ndege hiyo kwa muda ilikuwa haijulikani.

KQ inasema kwamba ndege hiyo ilipofika katika jimbo la Wajir uliopo kaskazini mashariki mwa Kenya, rubani wake aliombwa kuirejesha Nairobi , ambapo aliweza kutua salama katika uwanja wa JKIA mwendo wa saa tano na dakika arobaini na sita usiku wa Ijumaa bila ya tatizo kubwa.

Huku shirika hilo liliomba msamaha kwa yaliyojiri, lilitangaza pia kwamba abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo walikuwa wamepangiwa malazi kabla ya kuwekwa kwenye ndege nyingine jumamosi hii kuelekea Dubai.

KQ wiki hii imelazimika kujitetea baada ya vyombo vya Habari nchini Kenya kuandika tathmini ya malalamishi ya wateja kuhusu huduma zake na hatua za kampuni hiyo kuahirisha safari zake kwa wakati mfupi sana bila ya kuwapa wateja muda wa kutosha.

Chanzo: Bbc