Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege mbili zatunguliwa mapigano yakiendelea

Karthouom Sudan Ndege mbili zatunguliwa mapigano yakiendelea

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Majibu ya Haraka (RSF) kimetangaza kuwa kimetungua ndege mbili za kivita aina ya Sukhoi 24 mali ya jeshi la Sudan.

Habari hiyo imetangazwa huku mapigano makali yakiripotiwa kwa siku ya tatu mfululizo kati ya Jeshi la Akiba la Polisi ya Sudan na Vikosi vya Msajibu ya Haraka katika eneo la Al-Qaylab (kusini mwa Khartoum), kutokana na kutokuwepo makubaliano mapya ya kusitisha vita kati ya pande zinazozozana tangu kumalizika mapatano ya awali siku ya Jumatano iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na Kikosi cha Majibu ya Haraka (RSF) imeeleza kuwa kikosi hivyo vimetungua ndege za waliopanga mapinduzi kwa mara ya tatu katika muda usiozidi siku tatu.

Vyanzo vya habari pia vimeripoti mapigano makali na sauti ya milipuko katika mji mkuu wa Sudan huku ndege za kivita zikiendelea kushambulia baadhi ya maeneo ya mji huo.

Haitham Ibrahim, Waziri wa Afya wa Sudan, ametangaza kwamba hadi sasa mapigano hayo ya ndani yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000 na kujeruhiwa wengine 6,000.

Vita vya kuwania madaraka nchini Sudan ni baina ya jeshi la taifa la nchi hiyo linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan na Vikosi vya Majibu ya Haraka (RSF) chini ya uongozi wa naibu wake wa zamani, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live