Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege isiyo na rubani ya jeshi la Ethiopia yaua makumi ya watu

Ndege Isiyo Na Rubani Ya Jeshi La Ethiopia Yaua Makumi Ya Watu Ndege isiyo na rubani ya jeshi la Ethiopia yaua makumi ya watu

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Shambulio la ndege zisizo na rubani la jeshi la Ethiopia limeua makumi ya watu katika eneo la Amhara, kulingana na walioshuhudia na vyanzo vya hospitali.

Shambulio hilo liliripotiwa kutokea Jumatatu karibu na mji mdogo wa Sasit katikati mwa nchi wakati lori lilikuwa likiwashusha abiria.

Jeshi la Ethiopia limekuwa likipigana na kundi la wanamgambo wa eneo hilo liitwalo Fano tangu Aprili mwaka jana.

Wakazi waliambia BBC kuwa hadi raia 30, wakiwemo watu 16 wa familia moja waliokuwa wakirejea kutoka ubatizo wa mtoto mchanga, walipoteza maisha katika shambulio hilo.

Daktari alithibitisha kuwa watu 18 walipata majeraha mabaya na watatu kati yao walikufa walipofika katika kituo cha matibabu.

Mzozo huo ulizuka mwaka jana wakati mamlaka ilipoamua kuvunja kundi la wanamgambo lenye makao yake makuu ya kikabila na kuunganisha wanachama wake katika vikosi vingine vya usalama vya kikanda na kitaifa.

Serikali haijajibu ripoti za shambulio hilo la Jumatatu. Eneo la Amhara limekuwa katika hali ya hatari tangu Agosti mwaka jana.

Chanzo: Bbc