Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi za SADC kutumia Utalii kukuza uchumi

Faee52a1d4836b73dc9304b8eee465d4.png Nchi za SADC kutumia Utalii kukuza uchumi

Sun, 20 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAWAZIRI wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamepitisha itifaki ya kuendeleza utalii ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki jijini Dodoma wakati wa mkutano wa mawaziri wa SADC wanaohusika na mazingira, maliasili na utalii.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja alisema itifaki hiyo pia itaimarisha shughuli za utangazaji utalii na hivyo kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchi za SADC.

Aliwaeleza waandishi wa habari baada ya mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao kuwa, mawaziri hao pia wameridhia

kujiunga na mfuko wa mazingira ili kupata fedha za ufadhili kwa ajili ya utunzaji mazingira.

Masanja alisema katika mkutano huo masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na itifaki ya SADC ya usimamizi wa mazingira kwa ajili ya kujenga maendeleo endelevu, mikakati ya SADC na mabadiliko ya tabianchi na mpango kazi wa utekelezaji wake, kujiunga na mfuko wa mazingira, mkakati wa misitu wa SADC, mkakati wa SADC wa kudhibiti ujangili na itifaki ya kuendeleza utalii katika nchi hizo.

Alisema mawaziri wa SADC wamezihimiza nchi wanachama kuridhia itifaki ya SADC ya usimamizi wa mazingira kwa ajili ya kujenga maendeleo endelevu.

Alisema itifaki hiyo inalenga kuziwezesha nchi wanachama kunufaika na fursa za ufadhili wa programu zinazolenga kutunza

na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu.

“Mkutano pia umejadili na kupitisha mkakati wa SADC wa mabadiliko ya tabianchi na mpango kazi wa utekelezaji wake. Nchi

wanachama zimehimizwa kutekeleza mpango kazi huo na zimetaarifiwa kuhusu kuanzishwa kwa kamati maalumu ya wataalamu kwa ajili ya kuratibu masuala ya mabadiliko ya tabianchi pamoja na kupunguza athari za maafa,” alisema.

Masanja alisema Tanzania imekubali kuridhia ili ianze kutekeleza kwa manufaa ya taifa na Jumuiya ya SADC kwa ujumla.

“Ili kuwezesha kutekeleza jukumu la uhifadhi wa mazingira, mawaziri tumeridhia nchi wanachama wa SADC kujiunga na mfuko wa mazingira, kupitia mfuko huu nchi wanachama zitaweza kupata fedha za ufadhili kwa ajili ya kutunza na kuhifadhi

mazingira,” alisema Masanja.

Aidha, alisema katika kuhakikisha uhifadhi wa matumizi endelevu ya raslimali za misitu, kama mawaziri wa nchi wanachama wa SADC wamepitisha mkakati wa misitu wa SADC wa miaka 10 (2020-2030).

Alisema kupitia mkakati huo nchi wanachama zitakuza uwezo wa taasisi zinazosimamia raslimali za misitu, kukuza na kusimamia soko la biashara ya mazao ya misitu, kuchochea uwekezaji wa kifedha na ushiriki wa sekta binafsi na kuimarisha ulinzi na uongozaji wa maeneo ya misitu.

Alisema Tanzania imejenga ushirikiano na nchi wanachama katika kuhifadhi rasilimali wanyamapori na kwamba hatua hiyo

imewezesha kutekelezwa kwa mkakati wa pamoja wa kudhibiti ujangili wa miaka mitano 2016 hadi 2021.

“Baadhi ya mafanikio ambayo nchi wanachama wamenufaika kupitia mkakati huo ni kukua kwa ushirikiano baina ya nchi wanachama katika kudhibiti ujangili na biashara haramu ya nyara, ushirikiano kwenye kutoa mafunzo kwa maofisa wanyamapori kwa lengo la kujenga uwezo katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi wa raslimali anyamapori,” alisema.

Alisema pia nchi wanachama zimekuwa na mpango wa pamoja wa kusimamia maeneo ya hifadhi yanayovuka mipaka ili kuimarisha usimamizi wa rasilimali hizo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz