Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi za Magharibi zatajwa kufadhili ugaidi Afrika

Silaha Magharibi.jpeg Nchi za Magharibi zatajwa kufadhili ugaidi Afrika

Sat, 4 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ushahidi wa namna silaha haramu kutoka Ulaya zinavyoingia Afrika ulijitokeza mapema mwaka 2023. Silaha hizo haramu sasa si tu kuwa ziko mikononi mwa makundi makubwa ya kigaidi, bali pia zinatumiwa na makundi ya wanamgambo kwa ajili ya kujilinda.

Kwa mujibu wa duru za habari mtiririko wa silaha zinazosafirishwa kutoka Ulaya hadi Afrika tayari unaonyesha athari zake mbaya barani humo. Mashambulizi ya kigaidi katika maeneo ya kati na Kusini mwa Afrika yaliongezeka kwa asilimia 50 mwaka 2022 ikilinganishwa na miaka iliyopita huku ongezeko hilo likiwa ni asilimia 20 katika ukanda wa Afrika Magharibi. Silaha nyingi haramu zimehifadhiwa katika Bonde la Ziwa Chad na eneo la Sahel ya Kati.

Ismail Mohamed Tahir, mtaalamu wa masuala ya usalama wa Chad, anahofia kwamba mtiririko wa silaha za Ulaya barani Afrika utaendelea kuongezeka, na hii itachangia kuongezeka mivutano katika bara hilo.

Kulingana na mtaalam huyo wa Chad, eneo hilo limekuwa soko la wazi la biashara ya silaha kutoka Ulaya, ambazo aghalabu zinatoka Ukraine kupitia nchi za Ulaya.

Kulingana na Ofisi ya Kitaifa ya Upelelezi ya Finland (NBI), polisi wa nchi hiyo waligundua silaha za magendo kutoka Ukrainia zinazolekea barani Afrika Oktoba iliyopita. Kulingana na matokeo ya awali ya uchunguzi huo, ofisi hiyo imesema wahalifu wamepata idadi kubwa ya silaha ambazo hapo awali zilisafirishwa kwenda Ukraine kwa ajili ya vita dhidi ya Russia.

Eneo la Sahel limeshuhudia ongezeko kubwa la vurugu kati ya makundi ya kigaidi, ambayo yameongezeka mara nne tangu 2019. Na hakuna dalili kuwa hali hiyo itapungua mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live