Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi za EAC sasa zijipange kukabili ukame msimu wa vuli

830cae3c2c866fb1a94263feb6b05d8d Nchi za EAC sasa zijipange kukabili ukame msimu wa vuli

Tue, 15 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UTABIRI wa hali ya hewa kwa mvua za vuli kwa mwezi Oktoba, Novemba na Desemba mwaka huu katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki, umetolewa na kuonesha kuwa nchi hizo zitakabiliwa na hali ya ukame katika maeneo mengi.

Hali hiyo inatokana na upungufu wa mvua kutokana na mvua za wastani na chini ya wastani, jambo linalopaswa kila nchi kuhakikisha inajipanga vizuri kuhakikisha ukanda huu haupati madhara kutokana na ukame huo.

Ni dhahiri kuwa unapotolewa utabiri ambao kwa namna moja au nyingine unakuwa na uhakika kati ya asilimia 70 hadi 90 kwa jinsi msimu utakavyokuwa, unatoa fursa kwa nchi kujipanga ili kuepuka madhara yanayotokea kulingana na hali ya hewa.

Mamlaka za hali ya hewa kwa kila nchi zilivyotangaza utabiri na kubainisha kuwepo kwa upungufu wa mvua kwa pamoja, wamebainisha kuwepo kwa hali hiyo kutokana na viashiria kubainisha.

Katika msimu uliopita wa masika, ilishuhudiwa kuwepo kwa mvua nyingi ambazo licha ya kusababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao, zilisababisha majanga kwa nchi ya Rwanda.

Kati ya Januari na Aprili mwaka huu mvua hizo ziliathiri maisha ya watu 10 na kujeruhi 225. Nyumba 3,082 ziliiharibika na maelfu ya watu walikosa maeneo ya kuishi huku mifugo 3,000 ikifa.

Nchini Tanzania serikali imeeleza kuwa kuna chakula cha kutosha na imetaka wananchi kutumia na kuhifadhi vizuri chakula. Imesema kuna utoshelevu wa chakula kwa asilimia 124 na ziada ya tani za chakula milioni tatu, hivyo hakutakuwa na upungufu wa chakula.

Nchini Kenya katika mvua za masika kulikuwa na majanga ya uzalishaji wa chakula na wakati mwingine maeneo kadhaa yalivamiwa na nzige wekundu.

Katika msimu wa vuli maeneo mengi ya Kenya yanatarajiwa kushuhudia vipindi vya jua na hali ya ukavu mwezi Septemba, isipokuwa maeneo ya magharibi, Ziwa Victoria na yaliyo katikati ya Bonde la Ufa.

Kama ilivyo Kenya, utabiri kwa nchi zote za EAC unabainisha kuwepo kwa hali ya ukame, hivyo kila sekta inatakiwa kujipanga kukabiliana na hali hiyo kwa wakulima kufuata ushauri wa maofisa ugavi kwa kupanda mazao yanayostahimili ukame.

Katika kuhakikisha kinapatikana chakula cha kutosha, nchi za EAC zenye chakula cha kutosha ni vema ziweke mikakati ya matumizi mazuri, kwa kuepuka kutumia kiasi kikubwa katika pombe na masuala mengine. Nchi zote zinatakiwa kuhifadhi chakula kwa ajili ya kusambaza katika nchi jirani.

Chanzo: habarileo.co.tz