Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi za Afrika zinavyozungumzia shambulio la Israel

Mahakama Kenya Yakataa Ombi La Rais Ruto Kuhusu Kodi Nchi za Afrika zinavyozungumzia shambulio la Israel

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi kadhaa za Afrika zimeeleza wasiwasi wao baada ya shambulio la Iran dhidi ya Israel.

Afrika Kusini imesisitiza kwamba pande zote lazima “ziepuke kitendo chochote ambacho kitaongeza mvutano katika eneo hilo nyeti” na kusihi dunia isisahau vita huko Gaza.

“Afrika Kusini imekuwa ikisisitiza kwamba haijalishi kama nchi zinaamini kuwa matumizi yao ya nguvu ni halali, si busara kamwe kugeukia vita kwani kwa hakika, ni watu wa kawaida wanaoathirika zaidi na mzozo,” Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano ya Afrika Kusini ilisema.

Nigeria ilitoa wito kwa Iran na Israel “kuonyesha kiasi” na “kuepuka mgogoro mkubwa zaidi katika Mashariki ya Kati,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria ilisema.

“Katika kipindi hiki muhimu, ni jukumu la nchi hizi mbili kutafakari juu ya kujitolea kwa ulimwengu kwa utatuzi wa amani wa mizozo, kwa maendeleo ya amani na usalama wa kimataifa.”

Rais wa Kenya William Ruto alisema shambulio hilo “linazidisha hali ambayo tayari ni tete katika Mashariki ya Kati.”

Ruto alisema shambulio la Iran “linapaswa kulaaniwa na nchi zote zinazopenda amani” na kwamba Kenya “inaisihi Israel kuonyesha kiasi zaidi.”

Somalia ilitoa wito kwa pande zote “kusitisha kuongezeka kwa hali hiyo mara moja na kuonyesha kiasi cha juu,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia ilisema.

Wizara hiyo ilisema ongezeko la uhasama linatishia utulivu wa kikanda na usalama wa kimataifa, na kusisitiza hitaji la kusitisha vita huko Gaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live