Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi za Afrika zatakiwa kutokomeza ugaidi

Ubalozi Wa Ethiopia Nchini Sudan Waharibiwa Kwa Shambulio Nchi za Afrika zatakiwa kutokomeza ugaidi

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika (AU) umetoa wito kwa nchi za Afrika kutumia ushirikiano thabiti wa kiusalama ili kuzuia makundi ya kigaidi na kihalifu barani humo.

Wito huo wa dharura umetolewa na Alhaji Sarjoh Bah, mkurugenzi wa Usimamizi wa Migogoro ndani ya Idara ya Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama ya Umoja wa Afrika. Aidha amesisitiza haja ya kuweka juhudi za pamoja huku vitisho vya usalama vikiendelea kuibuka na kubadilika mara kwa mara katika sehemu tofauti za bara Afrika.

Mkurugenzi huyo wa AU alisema hayo wakati wa mkutano wenye mada ya amani na usalama, ambao ulifanyika Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania, kuanzia Novemba 5-7, ukiwa na msisitizo maalum wa kushughulikia vitisho vya usalama katika kanda za Sahel na Pembe ya Afrika.

Amesema, hali ya usalama katika maeneo hayo mawili ya Afrika inaendelea kuzorota, ikichangiwa na changamoto za kiutawala zinazoshuhudiwa katika baadhi ya nchi na kuzuka kwa mzozo nchini Sudan, na kusababisha ombwe la kisiasa na kiusalama na kuzua wimbi la wapiganaji wa kigeni na silaha. "

Ukanda wa Sahel Mkurugenzi huyo aliendelea kueleza wasiwasi wake kwamba makundi ya kigaidi yanaweza kuenea katika nchi za pwani na kuungana na makundi ya wahalifu wa kimataifa wanaojihusisha na uharamia na wizi wa kutumia silaha, pamoja na magenge ya magendo ya binadamu na biashara zingine haramu ili kufadhili operesheni zao.

Kwa mujibu wa AU, mkutano huo wa siku tatu, pamoja na mambo mengine, ulilenga kutafakari juu ya ongezeko la tishio la ugaidi na njia za kukabaliana na tatizo hilo kubwa.

Aidha mkutano huo umejadili mapatano juu ya mbinu za kuimarisha upashanaji habari na ushirikiano wa kiusalama huku pia ikibainisha njia za kusaidia nchi wanachama wa AU kushughulikia vitisho vilivyopo, na kukubaliana kwa pamoja kuhusu mbinu na ramani ya ushirikiano mwaka 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live