Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi za Afrika zajibu Vita Ukraine, Russia...

Wanajeshi Wa Ukraine Waharibu Ndege Mbili Zisizo Na Rubani Za Iran Nchi za Afrika zajibu Vita Ukraine, Russia...

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi za Kiafrika zimeyashutumu mataifa tajiri duniani kwa kupuuza mahitaji yao kwa ajili ya Ukraine, ambayo inasaidiwa kwa mabilioni ya dola.

Nchi za Kiafrika zimeeleza wasiwasi zilionao kutokana na unafiki na undumakuwili unaoonyeshwa na mataifa tajiri katika suala la misaada ya kimataifa.

Duru moja ndani ya serikali ya Zambia imesema, kuna mapigano na vita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan na maeneo mengine ya Afrika, lakini maeneo hayo hayasaidiwi kama ilivyo kwa Ukraine.

Aidha imeelezwa kuwa, msaada inaopata Ukraine hivi sasa kutoka nchi za Magharibi haujawahi kushuhudiwa na hauna mfano wake na hii inaonyesha kuwa, madola ya Maagharibi yamejikita zaidi tu katika kuziunga mkono nchi za Magharibi na kuwa na upendeleo katika hilo.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, soko la kimataifa la nafaka linakabiliwa na matatizo mengi kufuatia vita vya Ukraine. Russia na Ukraine ni miongoni mwa nchi zinazozalisha na kuuza kwa wingi nafaka duniani.

Mnamo Julai 22, 2022, Uturuki, Ukraine, Russia na Umoja wa Mataifa zilitiliana saini huko Istanbul hati ya kuwezesha kusafirishwa salama nafaka na chakula kutoka bandari za Ukraine. Makubaliano hayo yalirefushwa kwa muda wa miezi miwili Mei 17 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live