Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi 9 Afrika zateketeza chanjo ya corona 

Bee15519c8eb203e7dff1b967322d190 Nchi 9 Afrika zateketeza chanjo ya corona 

Sat, 17 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JUMLA ya dozi za chanjo 450,000 za virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covidi-19, zimeteketezwa katika nchi tisa za Afrika, kwa mujibu wa Shirika la Afrika Duniani (WHO).

Mkuu wa Chanjo na Maendeleo ya Chanjo katika ofisi ya WHO Kanda ya Afrika, Dk Richard Mihigo alisema jana kuwa, sababu ya hatua hiyo inatokana na chanjo ya AstraZeneca inayotumika sana Afrika usafirishwaji wake kuchelewa.

“Chanjo hizi hazikuharibiwa bure, ziliwasili zikiwa zimebakisha muda kidogo kabla ya kuharibika, hivyo ilikuwa ngumu kuzitumia,” alisema.

Alitaja nchi zilizoharibu chanjo hiyo kuwa ni Malawi, Sudan Kusini, Liberia, Mauritania, Gambia, Sierra Leone, Guinea, Comoro na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Malawi ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuteketeza chanjo hizo Mei 19, mwaka huu.

Waziri wa Afya nchini humo alieleza kuwa, hatua hiyo ilikuwa ni ya lazima ili kurejesha imani kwa wananchi.

“Hakuna nchi ambayo imejaribu kupoteza tu chanjo bila sababu,” alisema Dk Mihigo.

Ili kuepuka upotevu, nchi zinahimizwa kutumia chanjo mara moja zinapotolewa.

Nchi pia zinahimizwa kufanya kampeni za uhamasishaji pamoja na kampeni za chanjo nyingi ili jamii zijue umuhimu wa kupata chanjo hiyo.

Kati ya watu bilioni 1.2 barani Afrika, ni milioni nane pekee ndio wamepatiwa chanjo hiyo hadi sasa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz