Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nawaenjoi tu: Joshua Kutuny asema ataungana na DP Ruto wakati ukifika

935443f00da9f528 Nawaenjoi tu: Joshua Kutuny asema ataungana na DP Ruto wakati ukifika

Fri, 23 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu katibu wa Jubilee Joshua Kutuny amesema alishauriwa na wazee asiwahi isaliti jamii yakeAmesema kwa sasa yuko Jubilee kwa muda tu na baadaye atachukua mwelekeo mpya kisiasa Hatua yake huenda ikachochea masaibu ambayo yanazunguka chama cha Jubilee huku ikishukiwa wengi wa wafuasi wake ni wandani wa DP na wanasubiri muda tu na kisha kuungana naye kwenye IDAMbunge wa Cherangany Joshua Kutuny ameashiria atajiunga na NAibu Rais William Ruto kwenye chama chake cha UDA wakati bora ukifika.

Kutuny alisema yeye ni kijana ambaye huongozwa na ushauri wa wazee wa jamii na walimtaka asiwahi isaliti jamii yake.

"Wazee walinishauri nisiwahi isaliti jamii yangu, mimi Kutuny siwezi kuisaliti kabisa," Kutuny alisema kwenye mkutano katika eneo la Biribiriet.

Alitaka wafuasi wake wasiwe na wasiwasi kuhusu wadhifa wake kwa sasa ndani ya Jubilee ambapo ameonekana kuenda kinyume na kigogo wa Bonde la Ufa William Ruto.

Habari Nyingine: Jubilee Haiwezi Kuungana na ODM, Katibu Raphael Tuju Asema

Read also

Jubilee Haiwezi Kuungana na ODM, Katibu Raphael Tuju Asema

Kutuny alisema bado anapima hewa na wakati utafika ambapo ataondoka Jubilee na kuungana na Bonde la Ufa katika mwelekeo watakaochukua kisiasa.

"Watu wangu msijali kuhusu msimamo wangu kisiasa kwa sasa , niko hapo kwa muda tu," alisema Kutuny wakati wa mkutano huo.

Gavana wa Uaisn Gishu Jackson Mandago alisema hawana shida na alipo Kutuny lakini akamtaka kukoma kumshambulia DP kisiasa.



"Rafiki yangu Kutuny hatuna shida na wewe kuhusu ulipo kwa sasa kisiasa, apana ... shida yetu ni kuwa unamshambulia mtoto wetu DP," alisema Mandago.

Kutuny ndiye naibu katibu wa chama cha Jubilee wadhifa ambao alipata baada ya mwandani wa DP Ruto Caleb Kositany kufurushwa kutoka Jubilee.

Hatua yake ya kufungua roho kuhusu anayoamini kisiasa huenda ikageuka na kuwa mwiba kisiasa haswa ndani ya Jubilee.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.



Read also

Mbunge Mtarajiwa wa Kiambaa Aelezea Alivyotekwa Nyara na Kuvuliwa Nguo

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke