Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Navaa Kama Mama: Moses Kuria afichua vile amekua akihepa serikali Juja

7fa6e0fbf0a0494a Navaa Kama Mama: Moses Kuria afichua vile amekua akihepa serikali Juja

Wed, 5 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kuria alisema serikali inamhofia sana kwenye uchaguzi mdogo wa Juja kwani mikakati yake italeta ushindi kwa chama cha PEP

- Mgombea wa serikali ni mjane wa aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Francis Waititu, Susan Wakapee

- Kuria alisema ili asitiwe mbaroni na makachero waliowekwa kumuwinda inamlazimu avae buibui kila wakati

- uchaguzi huo unawakumbusha wanasiasa wa Kiambu ule wa 1997 ambapo Kuria alipanga njama ya mgombea 'hafifu' kumshinda Uhuru Kenyatta katika kinyang'anyiro cha Gatundu

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amesema serikali inahofia kichapo katika uchaguzi mdogo wa Juja.

Kuria alisema imekuwa vigumu kwake kukanyanga eneo bunge la Juja bila kuhangaishwa kwa kuwa na mgombea wa uchaguzi mdogo wa Mei 18 kupitia chama chake cha PEP.

Kuria naye kama sungura mjanja alisema amekuwa akiifunga macho serikali kwa kujifanya binti kila anapozuru eneo hilo.

"Serikali imenipiga marufuku nisikanyange Juja hata kama ni kukojoa. Sasa nimechoka kuvaa buibui kila wakati naingia humo ili wasinijue wanikamate," alisema Kuria.

Mbunge huyo anamuunga mkono mgombea George Koimburi wa PEP ambaye ni mshindani mkuu wa mwaniaji wa chama cha Jubilee Susan Wakapee.

Wakapee ni mjane wa aliyekuwa Mbunge Francis Waititu na anaungwa mkono na serikali katika kampeni zinazoongozwa na Gavana wa Kiambu Moses Kuria.

Kulingana na Kuria, serikali imeanza kutokwa na kijasho kwa kile anasema ni mgombea wake kuwa na umaarufu.

Jumanne Mei 4 Kuria alichapisha kura ya maoni aliyosema inafanywa kwa wapiga kura wa Juja na kuonyesha kuwa Koimburi ana umaarufu.

TUKO.co.ke hata hivyo haikuweza kuidhinisha uhalali wa kura hiyo iliyokuwa ikifanywa kupitia njia ya simu.

Mgombea huyo wa PEP amekuwa akijipata pabaya ikiwamo serikali kumwandama kutokana na madai kuwa ana karatasi feki za masomo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari za TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke