Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Natumai uchaguzi utakuwa wa amani – Guterres kwa DRC

Guterres Aendelea Kusisitiza Kusimamishwa Mapigano Gaza Natumai uchaguzi utakuwa wa amani – Guterres kwa DRC

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huku wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakiwa wanaingia kwenye uchaguzi mkuu wa rais, magavana, wabunge na madiwani, António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anatumai uchaguzi huo utafanyika kwa njia ya amani, uwazi na jumuishi.

Katibu Mkuu amelaani matukio ya ghasia yaliyoripotiwa wakati wa kampeni za uchaguzi na kuwasihi wanasiasa na wafuasi wao kujizuia kufanya vitendo vyovyote vile vinavyoweza kuchochea ghasia au kuibua kauli za chuki miongoni mwa jamii au makundi, hali kadhalika mashambulizi dhidi ya wagombea wanawake.

Guterres amevisihi vyama vyote vya siasa viwe makini katika matumizi ya maneno na vitendo vyao.

Amesisitiza msimamo wa Umoja wa Mataifa wa kuendelea kusaidia DRC kupitia Mwakilishi wake Maalum nchini DRC. Mwakilishi huyo ndiye pia Mkuu wa MONUSCO ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo.

Wakati huo huo Mkurugenzi MKuu wa Uhamiaji wa DRC (DGM) alitangaza Jumanne kwamba Mipaka ya nchi kavu, baharini na angani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) itafungwa leo Jumatano wakati nchi hiyo ikifanya uchaguzi mkuu. Kinshasa, mji mkuu wa DRC

Taarifa hiyo iliongeza kuwa safari za ndege za ndani zitasitishwa, isipokuwa kwa safari za kimataifa katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya nchi hiyo.

Uchaguzi wa rais, wabunge na mitaa unafanyika leo kote DRC.

Takriban wapiga kura milioni 44 waliojiandikisha wanatazamiwa kupiga kura katika taifa hilo kubwa la Afrika ya Kati lenye takriban watu milioni 100 katika uchaguzi huo.

Takriban watu 100,000 wanagombea katika kura hizo nne, huku Rais Felix Tshisekedi akitafuta muhula mwingine baada ya kushinda uchaguzi uliokuwa na utata mwaka 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live