Naibu Rais wa Kenya amesema anaona aibu kuwa inambidi aombe chakula huku kukiwa na uhaba wa chakula nchini humo.
"Nimetumia muda wangu wote, nikiwa na wageni, kuomba chakula. Wakiwemo wakoloni. Inadhalilisha. Lakini sina chaguo kwa sababu hatuwezi kuacha watu wetu wafe,” aliviambia vyombo vya habari vya ndani.
Naibu rais alisema kuwa ukosefu wa mvua kwa mfululizo umesababisha watu wengi kukosa chakula na wengine kufariki.
Alisema alikuwa amesali akiwa chini ya Mlima Kenya ili Mungu "aponye ardhi yetu" na kuwaokoa watu kutokana na janga hilo.
Akiongea na runinga ya lugha ya humu nchini, Bw Gachagua alisema kuombaomba kunachukizwa sana na jamii yake, akitaja kuwa ni kumdhalilisha mtoto wa mpigania uhuru wa zamani.